FPCT YAKUTANA NA BODI YA ELIMU
- Category: Education
- Date: 11-09-2021
Juni 28, Katibu Mkuu wa FPCT Mch. George Mwita alikutana na uongozi wa bodi ya Idara ya Elimu ya FPCT na Chuo cha Habari Maalum ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Lengo hasa la kikao hicho kilichodumu kwa takribani masaa 3, kilikuwa chenye lengo la kujadili na kupitia masuala mbalimbali yahusianayo na Chuo cha Habari Maalum kilichopo jijini Arusha.
Wajumbe waliohudhuria kikao hicho ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu FPCT Ndugu. Moses Suleiman, Mkuu wa Chuo cha Habari Maalum Mstaafu Dkt. Jackson Kaluzi, Mwenyekiti wa Bodi ya Idara ya Elimu Mhandisi. Jeremiah Bayaga na Mwenyekiti wa Chuo cha Habar